Mashabiki wakiwa wamekusanyika katika viunga vya
hospitali ya Muhimbili. Habari za awali ambazo kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Kinondoni Afande Kenyela amesema kuwa Kanumba alikuwa na kutoelewana
kati yake na Mpenzi wake ambazo taarifa za awali zinasema waligombana
na Kanumba alisukumwa na kugonga kichwa chini na mpenzi wake ambaye
ametambuliwa kwa jina moja la Lulu.
Habari ambazo bado Spoti na Starehe haijazithibitisha
zinasema kuwa Kanumba alikuwa akioga ili atoke na ndipo aliposikia
mpenzi wake akiongea na simu na mtu mwingine alipotoka kumuuliza ndipo
mzozo kati yao ukaanza na katika hali ya kusumunana Kanumba alisukumwa
akaanguka na kugonga kichwa chini.
Afande Kenyela alisema alipigiwa simu na ndugu wa
Kanumba ambaye walikuwa wakiishi pamoja na Kanumba na walipofika Pale
walikuta tayari ameshakata roho ila bado inasubiriwa ripoti ya daktari.
Kamanda Kenyela pia amesema kuwa mpenzi wak
e
Maerehemu Kanumba anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi. Lulu
ambaye naye anag’aa kwenye tasnia ya Filamu amekuwa akigonga vichwa vya
habari vya magazeti ya “udaku” kutokana na skendo za mara kwa mara za
mahusiano ya kimapenzi, ni majuzi tu mwanadada huyu ametimiza miaka 18
tangu kuzaliwa.
Aidha nyumbani kwa marehemu Sinza kumejaa ndugu jamaa
na marafiki kiasi barabara ya kwenda Lion kupitia Madukani inapitika
kwa taabu.
Kanumba ambaye alizaliwa mwaka 1984 amefanikiwa
kuzikonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya movie za Tanzania si tu kwa
Tanzania bali hata nje ya nchi pia. Kwa mashabiki wa filamu za kibongo
Kanumba alikuwa ni namba moja na kwa kiasi kikubwa aliweza kuweka
viwango kwani alikuwa anafaa kwa kila kona kuanzia kuigiza mpaka kuvaa
na adamu ya maisha tofauti na ma Super Star wengine hivyo kuwavutia watu
wa rika lote. Kanumba anamaliza kipindi chake cha miaka 28 akiwa
ameacha kumbukumbu ambayo itaishi kwa muda mrefu.
Mashabiki kupitia mitandao ya kijamii wameonyesha
masikitiko yao ambapo kufika saa tisa usiku habari zilikuwa zikisambaa
kama moto nyikani kupitia Facebook, Twitter na Blogs ikiwemo hii ya
Spoti na Starehe ambayo ilikuwa moja ya wa kwanza kupata habari.
|
No comments