BAADA YA KUKAMATWA WILFRED LWAKATARE CHADEMA WATAKA POLISI KUFANYA UCHUNGUZI
Siku
moja baada ya kukamatwa na kushikiliwa na vyombo vya usalama kwa
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) WILFRED LWAKATARE kwa tuhuma za kuhusika na mashambulizi ya
watu mbalimbali chama hicho kimelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi
wa suala hilo pasipo kuingiliwa na wanasiasa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ambao pia ulihudhuriwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. WILLBROAD SLAA amesema anashangazwa na hatua ya jeshi la polisi kumkamata kiongozi huyo wa CHADEMA kwa kuona picha kwenye mtandao wakati zipo taarifa nyingi za uchochezi zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii kuwahusu watu mbalimbali ambazo hazijachukuliwa hatua.
Amesema haamini kama kiongozi huyo wa CHADEMA anaweza kupanga mipango ya kufanya uvunjifu wa amani licha ya kuiona picha ya video iliyowekwa kwenye mtandao, ambayo amedai haina ushahidi wa kutosha.
Katika hatua nyingine Dk. SLAA amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipeleka malalamiko yao na vielelezo mbalimbali polisi kuhusu kuhujumiwa na watu wasiojulikana lakini mpaka sasa bado hakuna taarifa zozote za kiuchunguzi zilizofanywa na jeshi hilo.

No comments