Papa Francis kukutana na makadinali
Baba Mtakatifu Francis wa Kwanza anakutana na makadinali waliomchagua
kama Papa wa kwanza kuwahi kuongoza kanisa Katoliki kutoka Amerika ya
Kusini, wakati salamu za pongezi zikiendelea kumiminika kutoka kote
ulimwenguni. Jorge (KHORGE) Mario Bergoglio wa Argentina ameanza siku
yake ya kwanza kama Papa kwa kuhudhuria misa ya maombi katika kanisa la
Santa Maria Maggiore (MAJIORE) mjini Roma. Kisha Papa huyo mpya
akakwenda kuchukua mizigo yake kutoka chumba cha wageni katikati ya
Roma, ambako aliishi kabla ya kuanza kikao cha faragha cha baraza la
makadinali kupiga kura. Kisha anarudi tena katika kanisa dogo la Sistine,
kukutana na makadinali wenzake waliomchagua. Miongoni mwa waliotuma
salamu za pongezi ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon. Kesho
Ijumaa atakutana na makadinali wote wa Kanisa Katoliki, ikiwa ni pamoja na
wale wenye zaidi ya umri wa miaka 80.
No comments