Eti Francis wa kwanza ni Papa wa muda tu?
Papa Francis wa kwanza,kutokana na umri wake mkubwa na mwelekeo wake wa kihafidhina,haonyeshi kama atafanikiwa kulifanyia mageuzi kanisa katoliki,yanayoambatana na wakati tulio nao.
Wahenga wanasema mkamia maji hayanywi" hapa ikimaanisha anaeingia katika
mkutano wa siri akipewa nafasi nzuri ya kuchaguliwa kuwa Papa,anatoka
mkutanoni kama kadinali tu.Kwasababu hakuna yeyote kati ya waliopigiwa
upatu wangechaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa katoliki
ulimwenguni,aliyechaguliwa-badala yake makadinali wamemchagua mchamungu
ambae amejipatia umashuhuri kutokana na kutopenda makubwa pamoja na
juhudi zake za kuwapigania wasiojiweza .Kardinali wa ki-Argentina Jorge
Mario Bergoglio,aliyechagua jina la Francis wa kwanza,ni Papa wa kwanza
ambae hatokei Ulaya.Nchini mwake,amedhihirisha anapenda sana kuwa karibu
na watu na anazijua kikamilifu dhiki na shida za watu maskini.Hilo
pekee linawapa matumaini mema wakatoliki wanaoishi katika maene ya
mabanda,madongo poromoka na kambi za wakimbizi katika kila pembe ya
dunia.Katika eneo la Latin Amerika matumaini yalikuwa makubwa ya kumpata
Papa anaetambua hali zao za maisha.
Hata mrithi huyu wa sasa wa mjumbe wa Mungu Petrus ni mhafidhina- jambo
ambalo si la kustaajabisha - watangulizi wake wote wawili na kwa kipindi
cha miaka 35 iliyopita walikuwa wakiwachagua maaskofu wakuu wa
kihafidhina kuwa makadinali na kwa namna hivyo kuwapatia fursa ya
kumchagua Papa.Francis wa kwanza kwa hivyo hawezi kuwa mwanamageuzi
ambae wakosoaji wa kanisa wangependelea achaguliwe.Muumini huyo wa
madhehebu ya Jesuit anaitumia kila fursa inayojitokeza kukosoa kwa
maneno makali ukosefu wa usawa katika jamii-hata hivyo yeye mwenyewe
anatajikana kuwa karibu zaidi na jumuia ya wahafidhina sugu wa
kikatoliki:"Comunione e Liberazione".Theolojia ya ukombozi" haikuwa
shetani wake.Sasa jee Papa kama huyu anaweza kuyawekea suala la kuuliza
mafunzo ya dini ya kikatliki?
Na jee watu wanaweza kumpongeza Papa huyu?
Majukumu na matatizo yanayomsubiri mchamungu huyo mwenye umri wa miaka
76 ni makubwa kupita kiasi.Kwanza kabisa Papa Francis wa kwanza anabidi
arejeshe imani ya waumini.Kashfa ya kuingiliwa kimwili watoto na vijana
na wachamungu wa kikatoliki kimechafua sana hadhi ya kanisa na hasa
katika nchi za magharibi ambako umati wa waumini wanalipa kisogo kanisa.
Francis wa kwanza analazimika kuanzisha mageuzi yanayohitajika ya kanisa
na ambayo yalikuwa yaanze tangu zamani.Kuna suala la kuwepo tabaka
mbili za jamii kati ya maaskofu na watu wanaojitolea kulitumikia
kanisa,sura hiyo inabidi ibadilishwe na kuimarisha nafasi ya waumini
wanaolitumikia kanisa kwa kujitolea.Wakinamama, ambao ndio wanaotekeleza
sehemu kubwa ya shughuli za kanisa wanastahiki kuzingatiwa.Mjadala wa
uwazi kwa wale wanaounga mkono na wengine wanaopnga utawa unabidi
uendelezwe.Kitheolojia watu wanasubiri pia kuona vipi litashughulikiwa
suala la watu walioachana na kuowa au kuolewa na mtu mwengine.Uhusiano
pamja na makanisa ambayo si ya kikatoliki na hasa yale ya wapenda
mageuzi nao ia unahitaji kuchunguzwa.Mdahalo kati ya waumini wa dini
tofauti unabidi uendelezwe na mengi menginyo.
Si wa kumezewa mate
Lakini hata Vatikan kwenyewe kuna yanayobidi kushughulikiwa.Kashfa ya
kuibiwa hati za siri za Papa,visa vya kichini chini vya hadaa na
kutiliana fitna yote hayo yamezidisha dhana kwamba Papa Benedkt wa 16
alishindwa kuidhibiti hali ya mambo.
Hasha,hakuna anaeumezea mate wadhifa wa kiongozi wa wakatoliki bilioni
moja nukta mbili.Pekee umri wake mkubwa unamfanya mtu ashuku kama kweli
yeye ndie anaefaa.Yadhihirika zaidi kana kwamba makadinali wamemchagua
Papa wa kipindi cha mpito na wala hawajachagua mkonndo mpya.Pengine
mkutano wa siri,kutokana na hali inayolikabili kanisa katoliki
imeipoteza fursa iliyojitokeza.Lakini si kuna usemi usemao imani huzusha
miujiza.
No comments