Mchakato wa kumchagua Papa waanza
Mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani unaanza
leo wakati jopo la makadinali linapokutana rasmi kwa kazi hiyo, huku
swali linaloulizwa ikiwa safari hii pia Papa atatoka Ulaya au bara
jengine!
Wapo makadinali kadhaa ambao watu wameanza kuwafikiria, kama vile Schere
kutoka Brazil, Salazar Gomez wa Colombia na Turkson kutoka Ghana.
Lakini matakwa ya wengi ni kuwa na Papa kijana. Macho ya wengine
yanammulika Kadinali Joachim Meisner kuweza kushika nafasi hiyo kuwa
mrithi wa Kadinali Joseph Rätzinger - Papa Benedikti wa 16 .
Suala la Umri
Papa mpya anatakiwa awe mtu mwenye afya nzuri. Meisner ana umri
wa miaka 70 na ni mtu imara na msomi kama Rätzinger na msimamo wake ni
mchanganyiko wa Wojtyla yaani Papa John Paul wa pili na Rätzinger.
Rainer Maria Woelki ambaye ni mwenzake Meisner kutoka Berlin anasema
hakuna kosa ikiwa papa mpya atakua kati ya miaka 60 na 70. Askofu huyo
mkuu wa mji mkuu wa Ujerumani mwenyewe ana umri wa miaka 56 mmoja kati
ya wale walio vijana katika jopo la makardinali. Aprili 2005, jopo hilo
lilimchagua Kardinali Ratsinger kwa papa, siku tatu kabla ya kuadhimisha
miaka 78 tangu kuzaliwa.
Nafasi ya Ulaya
Papa atatokea tena Ulaya au bara lingine ikiwa na maana kwa mara ya
kwanza kuwa na Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani kutoka Afrika, Asia au
Amerika kusini ? Pia jee atatokana na kundi la waliobobea kwa elimu na
mwenye kuzungumza lugha kadhaa. Bila shaka hilo linaweza kuwa na
msisimko wa aina yake.
Kundi la Wataliani katika jopo hilo la viongozi 150 wa Kanisa ni lenye
nguvu likiwa na wajumbe 28 na huenda likaungana na wahafidhina kutoka
Uhispania na Ufaransa. Hata hivyo kuchaguliwa kwa Mtaliani si jambo la
uhakika kwa sababu Maaskofu nchini humo wamegawika katika makundi
kadhaa.
Majina kutoka Amerika Kusini na Afrika
Kutoka Amerika kaskazini na hasa Marekani si jambo
linalotarajiwa hata kidogo. Lakini majina yanayogonga vichwa vya habari
kutoka Amerika kusini ni pamoja na Askofu mkuu wa Sao Paulo Odilo Pedro
Scherer mwenye umri wa miaka 63 ambaye aliwahi kufanya kazi Vatikani kwa
miaka mingi. Nchi yake ni moja wapo ya zile muhimu miongoni mwa
Wakatoliki. Mwengine ni Ruben Salazar Gomez kutoka Colombia mwenye umri
wa miaka 70.
Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson ndiye mgombea pekee muhimu kutoka
bara la Afrika. Akiwa rais wa baraza la haki na amani la Kanisa Katoliki
ni mtu anayesifika panapohusika na kushughulikia maamuzi magumu.
Anazungumza lugha kadhaa na kuwa kivutio mpaka kwa Wajerumani.
Huenda kwa sasa, wakati jopo hilo likianza kukutana kesho, hakuna
aliyetokeza kuwa na nafasi ya kushinda moja kwa moja. Lakini Wakati
Benedikti wa XVI amejiuzulu kuwa Papa ,kuna usemi wa Kirumi usemao
"Entrare Papa et Uscire Cardinale," Anaiyengia kuwa Papa hutoka akiwa
tena Kardinali."
No comments