MOSHI MWEUSI WATOKA HII INA MAANA BADO PAPA HAJAPATIKANA
Moshi mweusi umetokea kwenye dari la hekalu ya
Sistine mjini Roma, hii inamaanisha kuwa makadinali walioko ndani ya
hekalu wameshindwa kuafikiana juu ya Papa mpya anayetarajiwa
kuchaguliwa.
Moshi mweupe utaashiria kupatikana kiongozi mpya wa kanisa Katoliki la Roma.
Makadinali hao wanatarajiwa kupiga kura mara nne kwa siku hadi pale theluthi mbili ya makadinali wote watakapoafikiana juu ya Papa mpya.
Walipiga kura yao ya kwanza ambayo haikuleta maafikiano jana usiku wa Jumanne. Yeyote atakayeteuliwa kuliongoza kanisa hilo katoliki anakabiliwa na wakati mgumu, ambapo kanisa limesongwa na kashfa mbali mbali pamoja na migawanyiko ya ndani.
Papa aliyeondoka Benedikt wa Kumi na sita aliwashangaza wengi alipotangaza kujiuzulu wadhifa huo, Alitoa sababu kuwa amezeeka na afya yake imedhoofika kwa hivyo haoni kuwa anaweza kutekeleza wajibu wake kikamilifu kama Papa wa kanisa.

No comments