Papa mpya huyu hapa
Jorge Mario Bergoglio kutoka Argentina ndiye Baba Mtakatifu mpya
atakayeliongoza kanisa katoliki baada ya kujulishwa hapo jana usiku kwa
ulimwengu. Kuanzia sasa anafahamika kama Baba Mtakatifu Francisco wa
Kwanza.
Baba Mtakatifu Francisco wa Kwanza mwenye umri wa miaka 76 alichaguliwa
hapo jana na makadinali 115 baada ya siku mbili ya uchaguzi na anamrithi
Benedict wa kumi na sita mabaye alijiuzulu mwezi uliopita. Papa huyo ni
wa 266 tangu kanisa hilo kuanzishwa miaka elfu mbili iliyopita na wa
kwanza kuchaguliwa kutoka Amerika ya Kusini na wa kwanza kutotoka barani
Ulaya tangu karne ya kumi na nane.
Franisco ni Jina kwanza kutumika
Papa mpya Jorge Bergoglio akiwa kati makadinali wengine
Jina lake Francisco pia ndiyo mara ya kwanza kutumika na papa.
Amekuwa kadinali wa Argentina tangu mwaka 1988 na amekuwa ktaika mstari
wa mbele katika usimamizi wa masuala ya kiutawala wa kanisa hilo na
hivyo kudhihirisha kuwa ataweza kutekeleza majukumu ya kuwa papa vyema.
Mwaka 2005 inasemekana aliibuka wa pili kwa wingi wa kura baada ya
Benedict wa 16. Papa Francisco wa kwanza amekuwa akijishughulisha sana
kuwafunza na kuwalea makasisi katika eneo la Amerika ya kusini ambalo
lina waumini wengi zaidi ya kote ulimwenguni na hilo kumfanya kuonekana
kumweka katika hali nzuri kuongoza kanisa Katoliki, na amelibadili sura
kanisa hilo katika eneo hilo la kihafidhina.
Aomba baraka za waumini
Muumini akipiga mayowe baada ya kutajwa Papa mpya
Katika hotuba yake ya kwanza katika ubaraza wa ghorofa ya
Basilica aliwaomba waumini kote duniani wa nia na kheri njema wamuombee
baraka na pia alimuombea Papa anayeondoka Benedikto wa Kumi na Sita.
Maelfu ya waumini tangu Jumanne wamekuwa wakikita kambi katika uwanja wa
mtakatifu Petro wakisubiri kuuona moshi mweupe ukifuka kutoka paa la
kanisa la Sisitine ambako Makadinali 115 walikuwa wamefungiwa hadi
wampate papa mpya na baada ya kupiga kura mara tano,jana usiku saa
moja,moshi mweupe ulionekana na kengele katika uwanja huo kupigwa huku
waumini hao wakishangilia kwa vifijo na nderemo.
Wengi walitumai kuwa kwa mara ya kwanza papa mtakatifu atatokea katika
eneo tofauti mbali na bara Ulaya huku kadinali kutoka Brazil Odilo
Sherer na kadinali kutoka Ufilipino wakipigiwa upatu.
Mjini Buenos Aires kulijaa shangwe punde tu baada ya Papa Francisco wa
kwanza kutangazwa kuwa papa mpya.Wengi walitumai kuwa kwa mara ya kwanza
papa mtakatifu atatokea katika eneo tofauti mbali na bara Ulaya huku
kadinali kutoka Brazil Odilo Sherer na kadinali kutoka Ufilipino
wakipigiwa upato.
Papa Francisco wa kwanza anaelezwa kuwa atakabiliwa na kibarua kigumu
cha kurejesha hadhi ya kanisa hilo ambayo imezongwa na kashfa za dhuluma
za kingono,ufisadi na malumbano ya wenyewe kwa wenyewe.
No comments